Zaburi 147:1-9
1
Msifuni Bwana. Tazama jinsi ilivyo vyema kumwimbia Mungu wetu sifa, jinsi inavyopendeza na kustahili kumsifu yeye!
2
Bwana hujenga Yerusalemu, huwakusanya Israeli walio uhamishoni.
3
Anawaponya waliovunjika mioyo na kuvifunga vidonda vyao.
4
Huzihesabu nyota na huipa kila moja jina lake.
5
Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.
6
Bwana huwahifadhi wanyenyekevu lakini huwashusha waovu mpaka mavumbini.
7
Mwimbieni Bwana kwa shukrani, mpigieni Mungu wetu kinubi.
8
Yeye huzifunika anga kwa mawingu, huinyeshea ardhi mvua, na kuzifanya nyasi kuota juu ya vilima.
9
Huwapa chakula mifugo na pia makinda ya kunguru yanapolia.
Settings