Mithali 9:8
Inaonyesha mstari 8 pamoja na muktadha unaouzunguka.
5
Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.
6
Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7
“Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha hukaribisha matukano; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.
8
Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
9
Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika.
10
“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
11
Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako.
Settings