Skip to content
Mithali 7:23-27

Mithali 7:23-27

23
mpaka mshale umchome ini lake, kama ndege anayenaswa kwenye mtego, bila kujua itamgharimu maisha yake.
24
Sasa basi wanangu, nisikilizeni; sikilizeni kwa makini nisemalo.
25
Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke, wala usitangetange katika mapito yake.
26
Aliowaangusha ni wengi; aliowachinja ni kundi kubwa.
27
Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini, ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 90 chars

Options