Mithali 5:3-6
3
Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4
lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.
5
Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.
6
Yeye hafikiri juu ya njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
Settings