Mithali 2:3-6
3
na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu,
4
na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
5
ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.
6
Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.