Chanzo na Thawabu ya Hekima
5
ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.
6
Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7
Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu, yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
8
kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
9
Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki na sawa: yaani kila njia nzuri.
10
Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako, nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
11
Busara itakuhifadhi na ufahamu utakulinda.
Settings