Mithali 2:1-6
1
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
2
kutega sikio lako kwenye hekima na kuweka moyo wako katika ufahamu,
3
na kama ukiita busara na kuita kwa sauti ufahamu,
4
na kama utaitafuta kama fedha na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
5
ndipo utakapoelewa kumcha Bwana na kupata maarifa ya Mungu.
6
Kwa maana Bwana hutoa hekima, na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
Settings