Mithali 16:25-33
25
Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini.
26
Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; njaa yake humsukuma aendelee.
27
Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao.
28
Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu.
29
Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya.
30
Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya.
31
Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu.
32
Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
33
Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa Bwana.
Settings