Hesabu 35:9-13
9
Kisha Bwana akamwambia Mose:
10
“Sema na Waisraeli, uwaambie: ‘Mtakapovuka Yordani kuingia Kanaani,
11
chagueni baadhi ya miji iwe miji yenu ya makimbilio, ambayo mtu ambaye ameua mwenzake bila kukusudia aweza kukimbilia humo.
12
Itakuwa mahali pa kukimbilia kutoka mlipiza kisasi, ili kwamba mtu aliyeshtakiwa kwa mauaji asife kabla ya kujitetea mbele ya mkutano.
13
Miji hii sita mtakayoitoa itakuwa miji yenu ya makimbilio.
Settings