Hesabu 21:10-20
10
Waisraeli waliendelea na safari yao na wakapiga kambi huko Obothi.
11
Kisha wakaondoka Obothi na kupiga kambi huko Iye-Abarimu, katika jangwa linalotazamana na Moabu kuelekea mawio ya jua.
12
Kutoka hapo waliendelea mbele wakapiga kambi kwenye Bonde la Zeredi.
13
Wakasafiri kutoka hapo na kupiga kambi kando ya Mto Arnoni, ambao uko katika jangwa lililoenea hadi nchi ya Waamori. Arnoni ni mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.
14
Ndiyo sababu Kitabu cha Vita vya Bwana kinasema: “…Mji wa Wahebu nchini Seifa na mabonde ya Arnoni,
15
na miteremko ya mabonde inayofika hadi mji wa Ari na huelekea mpakani mwa Moabu.”
16
Kutoka hapo waliendelea mbele hadi kisima cha Beeri; kwenye kisima ambacho Bwana alimwambia Mose, “Wakusanye watu pamoja, nami nitawapa maji.”
17
Kisha Israeli akaimba wimbo huu: “Bubujika, ee kisima! Imba kuhusu maji,
18
kuhusu kisima ambacho kilichimbwa na wakuu, ambacho watu mashuhuri walikifukua, watu mashuhuri wakiwa na fimbo za utawala na bakora.” Kisha wakatoka jangwani kwenda Matana,
19
kutoka Matana wakafika Nahalieli, kutoka Nahalieli wakafika Bamothi,
20
na kutoka Bamothi wakafika kwenye bonde lililoko Moabu, mahali ambapo kilele cha Pisga kinatazamana na nyika.
Settings