Mathayo 20:31-34
31
Ule umati wa watu ukawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti, wakisema, “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie.”
32
Yesu akasimama na kuwaita, akawauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”
33
Wakamjibu, “Bwana, tunataka kuona.”
34
Yesu akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.
Settings