Skip to content
Walawi 5:11-13

Walawi 5:11-13

11
“ ‘Ikiwa basi, hawezi kupata hua wawili au makinda mawili ya njiwa, ataleta sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Kamwe asiweke mafuta wala uvumba juu yake, kwa sababu ni sadaka ya dhambi.
12
Atauleta unga kwa kuhani, ambaye atachukua konzi moja kama sehemu ya kumbukumbu na atauteketeza kwenye madhabahu juu ya sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto. Hii ni sadaka ya dhambi.
13
Kwa njia hii kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yoyote ya hizo alizotenda, naye atasamehewa. Sadaka iliyobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyokuwa ile sadaka ya nafaka.’ ”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options