Skip to content
Yohana 5:31-40

Yohana 5:31-40

31
“Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
32
Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli.
33
“Mlituma wajumbe kwa Yohana, naye akashuhudia juu ya kweli.
34
Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa.
35
Yohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.
36
“Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma.
37
Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,
38
wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye.
39
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi.
40
Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options