Ayubu 40:9-13
9
Je, una mkono kama wa Mungu, nawe waweza kutoa sauti ya ngurumo kama yake?
10
Basi jivike mwenyewe utukufu na fahari, nawe uvae heshima na enzi.
11
Fungulia ukali wa ghadhabu yako, mtafute kila mwenye kiburi umshushe,
12
mwangalie kila mtu mwenye kiburi na umnyenyekeze, waponde waovu mahali wasimamapo.
13
Wazike wote mavumbini pamoja; wafunge nyuso zao kaburini.
Settings