Ayubu 33:12-18
12
“Lakini mimi ninakuambia, katika jambo hili wewe una makosa, kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mwanadamu.
13
Kwa nini unamlalamikia kwamba yeye hamjibu mwanadamu?
14
Kwa kuwa Mungu husema, wakati huu kwa njia moja, au wakati mwingine kwa njia nyingine, ingawa mwanadamu anaweza asielewe.
15
Mungu husema na mwanadamu katika ndoto, katika maono ya usiku, wakati usingizi mzito uwaangukiapo wanadamu wasinziapo vitandani mwao,
16
anaweza akasemea masikioni mwao, na kuwatia hofu kwa maonyo,
17
ili kumgeuza mtu kutoka kwenye kutenda mabaya na kumwepusha na kiburi,
18
kuiokoa nafsi yake na shimo, uhai wake usiangamizwe kwa upanga.
Settings