Skip to content
Yeremia 12:1-6

Yeremia 12:1-6

1
Wewe daima u mwenye haki, Ee Bwana, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi kwa raha?
2
Umewapanda, nao wameota, wanakua na kuzaa matunda. Daima u midomoni mwao, lakini mbali na mioyo yao.
3
Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!
4
Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “Bwana hataona yatakayotupata sisi.”
5
“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda, unawezaje kushindana na farasi? Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama, utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?
6
Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe: hata wao wamekusaliti; wameinua kilio kikubwa dhidi yako. Usiwaamini, ingawa wanazungumza mema juu yako.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options