Isaya 3:16-24
16
Bwana asema, “Wanawake wa Sayuni wana kiburi, wanatembea na shingo ndefu, wakikonyeza kwa macho yao, wanatembea kwa hatua za madaha, wakiwa na mapambo ya njuga kwenye vifundo vya miguu yao.
17
Kwa hiyo Bwana ataleta majipu kwenye vichwa vya wanawake wa Sayuni; Bwana atazifanya ngozi za vichwa vyao kuwa vipara.”
18
Katika siku ile Bwana atawanyangʼanya uzuri wao: bangili, tepe za kichwani, mikufu yenye alama za mwezi mwandamo,
19
vipuli, vikuku, shela,
20
vilemba, mikufu ya vifundo vya miguu, mshipi, chupa za manukato na hirizi,
21
pete zenye muhuri, pete za puani,
22
majoho mazuri, mitandio, mavazi, kifuko cha kutilia fedha,
23
vioo, mavazi ya kitani, taji na shali.
24
Badala ya harufu ya manukato kutakuwa na uvundo; badala ya mishipi, ni kamba; badala ya nywele zilizotengenezwa vizuri, ni upara; badala ya mavazi mazuri, ni nguo za magunia; badala ya uzuri, ni alama ya aibu kwa chuma cha moto.
Settings