Skip to content
Mwanzo 7:1-9

Mwanzo 7:1-9

1
Ndipo Bwana akamwambia Noa, “Ingia katika safina wewe na jamaa yako yote, kwa sababu katika kizazi hiki nimeona ya kuwa wewe ni mwenye haki.
2
Uchukue wanyama saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, na wanyama wawili wawili wa kila aina walio najisi wa kiume na wa kike.
3
Pia uchukue ndege saba walio safi wa kila aina, wa kiume na wa kike, ili kuhifadhi aina zao mbalimbali katika dunia yote.
4
Siku saba kuanzia sasa nitaleta mvua juu ya nchi kwa siku arobaini usiku na mchana, nami nitafutilia mbali kutoka uso wa nchi kila kiumbe hai nilichokiumba.”
5
Noa akafanya yote kama Bwana alivyomwamuru.
6
Noa alikuwa na miaka 600 gharika ilipokuja juu ya dunia.
7
Noa na mkewe na wanawe na wake zao wakaingia katika safina ili waepuke ile gharika.
8
Jozi ya wanyama walio safi na walio najisi, ndege na viumbe vitambaavyo,
9
wa kiume na wa kike, walikuja kwa Noa wakaingia katika safina kama Mungu alivyomwamuru Noa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options