Skip to content
Mwanzo 5:6-20

Mwanzo 5:6-20

6
Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7
Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
8
Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
9
Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10
Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
11
Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.
12
Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13
Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
14
Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.
15
Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16
Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
17
Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.
18
Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.
19
Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
20
Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options