Skip to content
Ezekieli 30:1-8

Ezekieli 30:1-8

1
Neno la Bwana likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, toa unabii na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Ombolezeni ninyi na mseme, “Ole wa siku ile!”
3
Kwa kuwa siku ile imekaribia, siku ya Bwana imekaribia, siku ya mawingu, siku ya maangamizi kwa mataifa.
4
Upanga utakuja dhidi ya Misri, nayo maumivu makuu yataijia Ethiopia. Mauaji yatakapoangukia Misri, utajiri wake utachukuliwa na misingi yake itabomolewa.
5
Kushi na Putu, Ludi na Arabia yote, Libya na watu wa nchi ya Agano watauawa kwa upanga pamoja na Misri.
6
“ ‘Hili ndilo Bwana asemalo: “ ‘Wale walioungana na Misri wataanguka na kiburi cha nguvu zake kitashindwa. Kutoka Migdoli hadi Aswani, watauawa ndani yake kwa upanga, asema Bwana Mwenyezi.
7
“ ‘Hizo nchi zitakua ukiwa miongoni mwa nchi zilizo ukiwa, nayo miji yao itakuwa magofu miongoni mwa miji iliyo magofu.
8
Ndipo watakapojua kwamba mimi ndimi Bwana, nitakapoiwasha Misri moto na wote wamsaidiao watapondwa.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options