Skip to content
Ezekieli 28:20-23

Ezekieli 28:20-23

20
Neno la Bwana likanijia kusema:
21
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Sidoni, ukatabiri dhidi yake,
22
nawe useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: “ ‘Mimi ni kinyume chako, ee Sidoni, nami nitapata utukufu ndani yako. Nao watajua kwamba Mimi ndimi Bwana, nitakapotekeleza hukumu zangu na kuonyesha utakatifu wangu ndani yake.
23
Nitapeleka tauni ndani yake na kufanya damu itiririke katika barabara zake. Waliochinjwa wataanguka ndani yake, kwa upanga dhidi yake kila upande. Ndipo watakapojua kwamba Mimi ndimi Bwana.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options