Skip to content
Ezekieli 25:1

Ezekieli 25:1

Inaonyesha mstari 1 pamoja na muktadha unaouzunguka.
1
Neno la Bwana likanijia kusema:
2
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya Waamoni utabiri dhidi yao.
3
Waambie, ‘Sikieni neno la Bwana Mwenyezi. Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Kwa sababu ulisema, “Aha!” juu ya mahali pangu patakatifu palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli ilipoangamizwa, na juu ya watu wa Yuda walipokwenda uhamishoni,
4
kwa hiyo nitawatia mikononi mwa watu wa mashariki mkawe mali yao. Watapiga kambi zao katikati yenu na kufanya makazi miongoni mwenu, watakula matunda yenu na kunywa maziwa yenu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options