Skip to content
Amosi 7:10-17

Amosi 7:10-17

10
Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote.
11
Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema: “ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga, na kwa hakika Israeli watakwenda uhamishoni, mbali na nchi yao.’ ”
12
Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako.
13
Usiendelee kutoa unabii katika Betheli, kwa sababu hapa ni mahali pa mfalme pa kuabudia na Hekalu la ufalme huu.”
14
Amosi akamjibu Amazia, “Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa mchungaji wa kondoo na mtunza mikuyu.
15
Lakini Bwana akanitoa kutoka kuchunga kondoo na kuniambia, ‘Nenda, ukawatabirie watu wangu Israeli.’
16
Sasa basi, sikieni neno la Bwana. Ninyi mnasema, “ ‘Usitabiri dhidi ya Israeli, na uache kuhubiri dhidi ya nyumba ya Isaki.’
17
“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana: “ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini, nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga. Shamba lako litapimwa na kugawanywa, na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani. Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni, mbali na nchi yao.’ ”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options