Skip to content
Matendo 24:5-9

Matendo 24:5-9

5
“Tumemwona mtu huyu kuwa ni msumbufu, anayechochea ghasia miongoni mwa Wayahudi duniani pote. Yeye ndiye kiongozi wa dhehebu la Wanazarayo,
6
na hata amejaribu kulinajisi Hekalu, hivyo tukamkamata; [tukataka kumhukumu kufuatana na sheria zetu.
7
Lakini jemadari Lisia alitujia na nguvu nyingi, akamwondoa mikononi mwetu,
8
akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako: ili] kwa kumchunguza wewe mwenyewe unaweza kujua kutoka kwake mambo yote tunayomshtaki kwayo.”
9
Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka yote haya ni kweli.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options