1 Wakorintho 3:18-23
18
Msijidanganye. Kama mtu yeyote miongoni mwenu akidhani kuwa ana hekima kwa viwango vya dunia hii, inampasa awe mjinga ili apate kuwa na hekima.
19
Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za Mungu. Kama ilivyoandikwa: “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao,”
20
tena, “Bwana anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.”
21
Hivyo basi, mtu asijivune kuhusu wanadamu! Vitu vyote ni vyenu,
22
ikiwa ni Paulo au Apolo au Kefa au dunia au uzima au mauti, au wakati uliopo au wakati ujao, haya yote ni yenu
23
na ninyi ni wa Kristo, naye Kristo ni wa Mungu.
Settings