Zaburi111
Listen to this chapter
0:00
0:00
Ahadi ya Kumsifu Mungu kwa Moyo Wote
1
Msifuni Bwana. Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
Ukuu wa Matendo ya Mungu
2
Kazi za Bwana ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3
Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima.
4
Amefanya maajabu yake yakumbukwe, Bwana ni mwenye neema na huruma.
Mungu Hutoa Mahitaji na Agano Lake la Milele
5
Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele.
6
Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine.
7
Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika.
8
Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9
Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
Mwanzo wa Hekima
10
Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa zake zadumu milele.
Settings
Reading style
Typeface
Font size px
Reading width chars
Options
Study note