Skip to content
Zaburi 55:1-8

Zaburi 55:1-8

1
Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi. Ee Mungu, sikiliza maombi yangu, wala usidharau hoja yangu.
2
Nisikie na unijibu. Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
3
kwa sauti ya adui, kwa kukaziwa macho na waovu, kwa sababu wananiletea mateso juu yangu na kunitukana kwa hasira zao.
4
Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia.
5
Woga na kutetemeka vimenizunguka, hofu kuu imenigharikisha.
6
Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa! Ningeruka niende mbali kupumzika.
7
Ningalitorokea mbali sana na kukaa jangwani,
8
ningaliharakisha kwenda mahali pa salama, mbali na tufani kali na dhoruba.”
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options