Zaburi 33:1-4
1
Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki; kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
2
Msifuni Bwana kwa kinubi, mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.
3
Mwimbieni wimbo mpya; pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.
4
Maana neno la Bwana ni haki na kweli, ni mwaminifu kwa yote atendayo.