Skip to content
Hesabu 3:6-19

Hesabu 3:6-19

6
“Walete watu wa kabila la Lawi mbele ya Aroni kuhani ili wamsaidie.
7
Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.
8
Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.
9
Wakabidhi Walawi kwa Aroni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.
10
Waweke Aroni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu ni lazima auawe.”
11
Bwana akamwambia Mose,
12
“Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,
13
kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Bwana.”
14
Bwana akamwambia Mose katika Jangwa la Sinai,
15
“Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”
16
Kwa hiyo Mose akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Bwana.
17
Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
18
Haya ndiyo yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.
19
Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
Settings

Reading style

Typeface

Font size 19px

Reading width 75 chars

Options