Marko 13:35-37
35
“Basi kesheni kwa sababu hamjui ni lini mwenye nyumba atakaporudi: iwapo ni jioni, au ni usiku wa manane, au alfajiri awikapo jogoo, au mapambazuko.
36
Kama akija ghafula, asije akawakuta mmelala.
37
Lile ninalowaambia ninyi, nawaambia watu wote: ‘Kesheni!’ ”