Skip to content
Walawi 19:26-31

Walawi 19:26-31

26
“ ‘Msile nyama yoyote yenye damu ndani yake. “ ‘Msifanye uaguzi wala uchawi.
27
“ ‘Msikate nywele za kichwa denge, wala kunyoa pembe za ndevu zenu.
28
“ ‘Msichanje chale miili yenu kwa ajili ya mfu, wala msijichore alama juu ya miili yenu. Mimi ndimi Bwana.
29
“ ‘Usimdhalilishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo nchi itageukia ukahaba na kujaa uovu.
30
“ ‘Shika Sabato zangu na kuheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Bwana.
31
“ ‘Msiende kwa waaguzi, wala msitafute wapunga pepo, kwa maana watawanajisi. Mimi ndimi Bwana Mungu wako.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options