Skip to content
Walawi 11:2-8

Walawi 11:2-8

2
“Waambieni Waisraeli: ‘Kati ya wanyama wote waishio juu ya nchi, hawa ndio mtakaowala:
3
Mwaweza kula mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika sehemu mbili na ambaye hucheua.
4
“ ‘Kuna wanyama wengine ambao hucheua tu au wenye kwato zilizogawanyika tu, lakini hao kamwe msiwale. Ngamia ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; kwa kawaida ya ibada hiyo ni najisi kwenu.
5
Pelele ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.
6
Sungura ingawa hucheua hana kwato zilizogawanyika; huyo ni najisi kwenu.
7
Naye nguruwe ingawa anazo kwato zilizogawanyika sehemu mbili, hacheui; huyo ni najisi kwenu.
8
Kamwe msile nyama yao wala kugusa mizoga yao; wao ni najisi kwenu.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options