Isaya 19:5-10
5
Maji ya mito yatakauka, chini ya mto kutakauka kwa jua.
6
Mifereji itanuka; vijito vya Misri vitapungua na kukauka. Mafunjo na nyasi vitanyauka,
7
pia mimea iliyoko kando ya Mto Naili, pale mto unapomwaga maji baharini. Kila shamba lililopandwa kando ya Mto Naili litakauka, litapeperushwa na kutoweka kabisa.
8
Wavuvi watalia na kuomboleza, wale wote watupao ndoano katika Mto Naili, watadhoofika kwa majonzi.
9
Wale watu wafanyao kazi ya kitani kilichochambuliwa watakata tamaa, wafumaji wa kitani safi watavunjika moyo.
10
Wafanyao kazi ya kufuma nguo watahuzunishwa, nao vibarua wataugua moyoni.
Settings