Skip to content
Mwanzo 7:17-24

Mwanzo 7:17-24

17
Kwa siku arobaini mafuriko yaliendelea kujaa duniani na maji yalivyozidi kuongezeka, yaliinua safina juu sana kutoka kwenye uso wa nchi.
18
Maji yakajaa na kuongezeka sana juu ya nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.
19
Maji yakazidi kujaa juu ya nchi, yakaifunika milima yote mirefu chini ya mbingu yote.
20
Maji yakaendelea kujaa yakaifunika milima kwa kina cha zaidi ya dhiraa kumi na tano.
21
Kila kiumbe hai kitambaacho juu ya nchi kikaangamia: Ndege, wanyama wa kufugwa, wanyama pori, viumbe vyote juu ya nchi na wanadamu wote.
22
Kila kiumbe juu ya nchi kavu chenye pumzi ya uhai kikafa.
23
Kila kitu chenye uhai juu ya uso wa nchi kilifutiliwa mbali, watu, wanyama, viumbe vitambaavyo na ndege warukao angani wakafutiliwa mbali toka duniani. Waliobaki ni Noa peke yake na wale waliokuwa pamoja naye ndani ya safina.
24
Maji yakaifunika dunia kwa siku 150.
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options