Skip to content
Kumbukumbu 1:9-13

Kumbukumbu 1:9-13

Musa Ateua Viongozi na Waamuzi

9
Wakati ule niliwaambia, “Ninyi mmekuwa mzigo mzito sana kwangu kuwachukua peke yangu.
10
Bwana Mungu wenu ameongeza hesabu yenu, hivi kwamba leo ninyi ni wengi kama nyota za angani.
11
Naye Bwana, Mungu wa baba zenu na awaongeze mara elfu na kuwabariki kama alivyoahidi!
12
Lakini mimi nitawezaje kubeba matatizo yenu, na mizigo yenu, na magomvi yenu peke yangu?
13
Chagueni baadhi ya watu wenye hekima, wenye ufahamu na wanaoheshimika kutoka kila kabila lenu, nami nitawaweka juu yenu.”

Jifunze kifungu hiki

Ufafanuzi wa kifungu hiki, si mstari mmoja.

Maandiko mengine yanaposema hivi.

  • Zaburi 115:14

    Bwana na awawezeshe kuongezeka, ninyi na watoto wenu.
    kutoka mstari wa 11
  • Mwanzo 22:17

    hakika nitakubariki, na nitauzidisha uzao wako kama nyota za angani na kama mchanga ulioko pwani. Wazao wako watamiliki miji ya adui zao,
    kutoka mstari wa 10
  • Mwanzo 26:4

    Nitafanya wazao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa nchi hizi zote na kutokana na uzao wako mataifa yote yatabarikiwa,
    kutoka mstari wa 11
  • Kutoka 18:21

    Lakini uchague watu wenye uwezo miongoni mwa watu wote, watu wanaomwogopa Mungu, watu waaminifu wanaochukia mali ya dhuluma, uwateuwe wawe maafisa juu ya maelfu, mamia, hamsini na makumi.
    kutoka mstari wa 13
  • Hesabu 6:27

    “Hivyo wataliweka Jina langu juu ya Waisraeli, nami nitawabariki.”
    kutoka mstari wa 11
  • Kutoka 18:18

    Wewe pamoja na watu hawa wanaokujia mtajichosha bure. Kazi ni nzito sana kwako, huwezi kuibeba mwenyewe.
    kutoka mstari wa 9
  • 2 Samweli 24:3

    Lakini Yoabu akamjibu mfalme, “Bwana Mungu wako na azidishe jeshi mara mia, nayo macho ya bwana wangu mfalme na yaone hili. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme anataka kufanya kitu cha namna hii?”
    kutoka mstari wa 11
  • Mwanzo 49:25

    kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia, kwa sababu ya Mwenyezi, yeye anayekubariki kwa baraka za mbinguni juu, baraka za kilindi kilichoko chini, baraka za matitini na za tumbo la uzazi.
    kutoka mstari wa 11
  • Kumbukumbu 10:22

    Baba zako walioshuka kwenda Misri jumla yao walikuwa sabini, na sasa Bwana Mungu wako amekufanya wengi kama nyota za angani.
    kutoka mstari wa 10
  • Kutoka 32:13

    Wakumbuke watumishi wako Abrahamu, Isaki na Israeli, ambao uliwaapia kwa nafsi yako mwenyewe: ‘Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama nyota za angani, nami nitawapa wazao wako nchi hii yote ambayo niliwaahidia, nayo itakuwa urithi wao milele.’ ”
    kutoka mstari wa 10
  • Mwanzo 15:5

    Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”
    kutoka mstari wa 10
  • Hesabu 22:12

    Lakini Bwana akamwambia Balaamu, “Usiende pamoja nao. Hupaswi kulaani watu hao, kwa kuwa wamebarikiwa.”
    kutoka mstari wa 11
Settings

Reading Style

Typeface

Font Size 19px

Options