1 Wafalme 1:50-51
50
Lakini Adoniya kwa kumwogopa Solomoni, akaenda na kushika pembe za madhabahu.
51
Kisha Solomoni akaambiwa, “Adoniya anamwogopa Mfalme Solomoni na ameshikilia pembe za madhabahu. Anasema, ‘Mfalme Solomoni na aniapie leo kwamba hatamuua mtumishi wake kwa upanga.’ ”