Zaburi14
Listen to this chapter
0:00
0:00
Mpumbavu Amkataa Mungu
1
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Mpumbavu anasema moyoni mwake, “Hakuna Mungu.” Wameharibika, matendo yao ni maovu kabisa; hakuna hata mmoja atendaye mema.
2
Bwana anawachungulia wanadamu chini kutoka mbinguni aone kama wako wenye akili, wowote wanaomtafuta Mungu.
3
Wote wamepotoka, wameharibika wote pamoja, hakuna atendaye mema. Naam, hakuna hata mmoja!
Hukumu juu ya Watenda Maovu
4
Je, watendao mabaya kamwe hawatajifunza: wale ambao huwala watu wangu kama watu walavyo mkate, hao ambao hawamwiti Bwana?
5
Wako hapo, wameingiwa na hofu kuu, maana Mungu yupo pamoja na wenye haki.
6
Ninyi watenda mabaya mnakwamisha mipango ya maskini, bali Bwana ndiye kimbilio lao.
Maombi ya Wokovu wa Israeli
7
Laiti wokovu wa Israeli ungalikuja kutoka Sayuni! Wakati Bwana arejeshapo wafungwa wa watu wake, Yakobo na ashangilie, Israeli na afurahi!
Settings
Reading style
Typeface
Font size px
Reading width chars
Options
Study note